Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 15 YA 31

Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja (m.17-18). Mfano huu unawahusu Wayahudi jinsi walivyoupokea wito wa Mungu uliotolewa kwa njia ya Yesu. Na mfano huu pia unatuhusu sisi! Ni jinsi gani sisi tunavyoupokea wito wa Mungu wa kuingia katika ufalme wake? Kengele ya kanisa inapolia Jumapili ili kutuita twende kusali, je, tunaitikia vipi? Angalia udhuru unaotolewa kwa nia moja katika m.18-20: Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ng'ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja! Je, wewe unatoa udhuru unaofanana na hizi? Kwa kweli ni jambo la ajabu kutojali mwaliko wa Mungu. Ni hatari!

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz