Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Kuanzia 15:3 Yesu amejibu manung’uniko ya Mafarisayo. Lakini badala ya kupokea mafundisho yake na kutubu, wakaanza kumdhihaki, maana waliguswa rohoni na maneno yake aliyowaambia akisema, Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili (m.13). Tangu Yesu alipokuja, majira mapya yamekuwepo kwa Wayahudi, kwani ufalme wa Mungu umekaribia: Tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu (m.16). Wengi wasiojidai haki mbele ya watu (yaani hufanya kinyume na Mafarisayo ambao walijidai haki mbele ya wanadamu; m.15) wamefurahia habari hii jema na kumsikiliza Yesu kwa hamu. Ila Mafarisayo hawafurahi, ndiyo maana wakasema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao (15:2). Hata wameitafakari torati isivyo halali. Mfano mmoja ni ndoa. Ila Yesu anasisitiza maana yake, akisema, Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini (m. 18)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz