Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 25 YA 31

Unapata picha gani ya Yesu unapowaza juu ya Krismasi? Kwa wengi wanamwona kama mtoto mchanga aliyezaliwa horini kwa kukosa nafasi kwenye hotefi safi. Somo la leo linatoa picha tofauti: Yesu ni Mungu (m.1, Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu), Muumbaji (m.3, Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote), tena mtoa uzima (m.4, Ndani yake mdimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu). Yesu ni nuru ambayo yang’aa gizani wala giza halikuiweza (yaani, halikuweza kuishinda; m.5). Tusherehekee Krismasi tukijua kuwa ndani yetu tunaomwamini Yesu, yuko yeye aliyeshinda giza la ulimwengu huu.

Andiko

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz