Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 27 YA 31

Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, … (m.2). Jiwe la kusagia lilikuwa zito sana. Kutupwa baharini katika hali hiyo ni sawa na kufa. Kwa maneno haya makali Yesu anataka kusisitiza ubaya wa tendo la kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa (m.2). Ni nani? Labda anafikiria watoto. Kumbuka Yesu anavyosema katika Mt 18:5-6, Ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi; bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari. Au pengine Yesu anamaanisha wanafunzi wake, maana mtu hawezi kuingia katika Ufalme wake bila kuwa kama mtoto mdogo. Ndivyo Yesu anavyoeleza katika Mt 18:3-4, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni (Mt 18:3-4). Siku nyingine Yesu alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. Hili ni onyo kwa Mafarisayo, na kwetu pia!

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz