Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Siku ya pili ya Krismasi inaitwa siku ya kukumbuka wale waliofia dini, yaani, wale waliouawa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu. Neno la leo linatuangaliza kuwa tunapokwenda kuhubiri Injili, tutegemee pia upinzani. Biblia ina mifano ya wengi waliouawa kwa kumtangaza Kristo. Pia historia ya kanisa imetoa mifano ya namna hiyo. Kwa nini? Angalia anayosema Yesu katika m.37, Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka! Yesu anataka kuwaokoa hata wale wanaomwasi. Hivyo na sisi tuwe tayari kutoa maisha yetu kwa ajili ya Injili, ikibidi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz