Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 29 YA 31

Mungu ni msaada kwa wote wamwitao. Jambo pekee la somo ni kuonyesha kuwa baraka za Mungu hazitenganishwi na hali yetu mbele zake. Angalia jinsi hali hiyo inavyofungamana na imani yetu, wakati vitendo vyetu ni tokeo tu la imani. Kwanza na hata mwisho Daudi anamtegemea Mungu na ahadi zake. Katika m.18 anasema, Bwana alikuwa tegemeo langu; na katika m.30 anasema, Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya Bwana imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia. Kwa hiyo anazishika njia za Mungu na kukataa uovu. Muumini atendaye hivyo ni mkamilifu, wakati mpotovu ni huyu anayeacha njia za Mungu kwa kuwa hamtegemei. Mtu huyo asitegemee msaada wowote. Daudi anahitimisha, Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu; Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi (m.25-26).

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz