Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Kwanza inaelezwa Mungu alivyo (m.31: Ni nani aliye mwamba ila Mungu wetu?) na yale afanyayo: Umenipa ngao ya wokovu wako, Mkono wako wa kuume umenitegemeza, Na unyenyekevu wako umenikuza. Umezifanyizia nafasi hatua zangu (m.35-36a). Halafu inaelezwa yale aliyofanya Daudi baada ya kutiwa nguvu na Mungu: Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu, Naye anaifanya kamilifu njia yangu. Miguu yangu anaifanya kuwa ya kulungu, Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. Ananifundisha mikono yangu vita, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba (m.32-34). Mfuatano huu watukumbusha nini? Mungu akifanya kazi pamoja na waumini, hawajisikii wenye nguvu, bali kila wakati wanakumbushwa kwamba mwenye nguvu ndiye Mungu. Angalia pia lengo la Mungu kututia nguvu. Ni kuzifanya njia zetu ziwe kamilifu (m.32, Mungu ... anaifanya kamilifu njia yangu). Hatupewi nguvu ya kufanya tupendavyo sisi, bali ni muhimu kujikabidhi kwa ahadi zake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz