Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 28 YA 31

Katika zaburi hii, Daudi anakumbuka matendo makuu aliyotendewa na Mungu kwa nyakati na mazingira tofauti. Ukiwa na muda, soma k.mf. kuhusu Wafilisti katika 1 Sam 23:1-5 na kuhusu Sauli katika 1 Sam 24, 26 na 27:1. Daudi akiyakumbuka hayo yote yaliyotokea katika maisha yake, anakiri kuwa nguvu za Mungu ndizo zilizomwokoa. Mungu pekee ndiye awezaye kutusaidia na sisi, na kutuokoa siku za shida. Katika m.6 anakiri kwa kusema, katika shida yangu nalimwita Bwana, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake. Hii inaonesha ilivyo na maana kumwomba Mungu wakati wote bila kukoma, na kumbuka Mungu awezavyo kutumia hata nguvu za uumbaji anapokujibu. Tafakari anachosema Daudi, Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikasuka-suka; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu … Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee Bwana, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako (m.7-15).

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz