Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Krismasi ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Mungu anajifunua kwetu kwa njia ya Yesu Kristo ambaye ni mng’ao wa utukufu wake. Maana yake, mtu aliyemwona Yesu amemwona Mungu. Somo la leo linatukumbusha lengo la Yesu kuja. Mungu amemweka kuwa mrithi wa yote. Hivyo Yesu anakuja ili atutakase dhambi zetu ili na sisi tupate kibali cha kung’aa mbele za Mungu kama yeye alivyo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz