Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 23 YA 31

Dhambi daima inaathiri maisha yetu ya wokovu, na tukiendelea na hiyo dhambi bila kuitubia, itaharibu kabisa uzima wetu. Daudi aliliona hilo, ndiyo maana anamwomba Mungu amrudishie hali yake ya awali ya kuishi na Mungu ili apate kuwafundisha wakosaji wengine njia ya kurejea kwa Mungu. Anasema, Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu. Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako ... Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako (m.10-13). Tunafundishwa kutubia dhambi zetu na kuishi maisha ya kujiepusha na dhambi. Tumwombee Mungu atusaidie kuona makosa yetu na kumkimbilia Yesu kwa toba ili atusafishe na kututangazia msamaha. Yesu akamwambia [yule mwanamke], Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia, Hakuna, Bwana.Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena (Yn 8:10-11).

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz