Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 22 YA 31

Daudi alifanya dhambi ya zinaa na mke wa Uria, na baadaye alimwua Uria ili kuficha aibu. Hata hivyo Mungu alifichua kabisa dhambi yake (unaweza kujisomea habari zote katika 2 Sam 11:1-12:7). Tunaona huzuni ya Daudi baada ya kutambua dhambi yake. Anaomba fadhili za Mungu ili makosa yake yafutwe: Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima (m.1-3). Tunajifunza kwamba tusifiche dhambi. Dawa ya dhambi ni kutubu, kwani Yesu alikuja ulimwenguni kutafuta na kuokoa waliopotea (Lk 19:10). Fikiria, Daudi alisamehewa dhambi zake mbaya sana! Nawe utasamehewa ukitubu!

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz