Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Huwa watu katika mifano ya Yesu hawana majina. Kwa kumpa jina yule maskini, Yesu anatuambia jambo muhimu juu yake. Maana ya jina ”Lazaro” ni ”Mungu anasaidia”. Huenda Yesu anampa jina hili kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu katika umaskini wake. Au anataka kutuonyesha kwamba Mungu daima yuko upande wa walioonewa. Ingawa Lazaro alimtumaini Mungu hakupata nafuu kwanza. Ilikuja baadaye. Tunajifunza mawaili: 1. Tusichoke kumtumaini Mungu (jisomee k.mf. Zab 34:1-8, 17-22)! 2. Tujali sana Neno la Mungu. Zingatia jibu la Ibrahimu katika m.28-31, yule tajiri anamwambia, Baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz