Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 19 YA 31

Leo Yesu hutufundisha mambo mawili: 1. Tusiwe watumwa wa mali. Mtu anayelenga kuongeza tu mali yake, hawezi kumtumikia Mungu, maana mali imekuwa bwana wake. Hata atajaribiwa kutumia udhalimu ili kuongeza mali yake. Ndivyo Yesu anavyokumbusha katika m.10-12: Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe (m.10-12; ukipenda, linganisha na 1 Tim 6:7-10). Lakinini ijulikane kuwa hamwezi kumtumikia Mungu na mali (m.13). 2. Tutumie mali yetu, vyote tulivyo navyo, kwa kumtumikia Mungu. Tusiige udhalimu wa yule wakili mbaya, bali tuwe na ukarimu. Tujifunze busara ya kujifanyia rafiki ili wapate kumjua Yesu. Ni jambo la kudumu!m.9 unaeleza vizuri: Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz