Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Wayahudi walipofundisha kwa njia ya mifano daima ilihusu wanaume. Yesu aliwainua wanawake na kuwapa nafasi. K.mf. jana tulipata mfano mmoja uhusuo mwanamke! Ndipo leo twasoma mfano wa mwana mpotevu. Ni mfano mzuri sana wa habari njema aliyohubiri Yesu. Alivyotenda huyo baba si kawaida katika mazingira ya Kiyahudi na Kiarabu. Ila Mungu ni tofauti na wanadamu! Hata ukiwa umepotea sana, atakuwa amefurahi mno ukirudi kwake! Amejaa huruma na kweli (ndivyo Yohana alivyoona alipomtazama Yesu. Anashuhudia, Tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli; Yn 1:14)! Yule mwana wa pili ni mfano wa Mafarisayo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz