Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 16 YA 31

Jana tuliona kwamba kuingia katika Ufalme wa Mungu hakutegemei ustahili wa mtu bali mwaliko wa Mungu ambao unakwenda kwa watu wote. Hata mtu asiyeheshimika na watu, kwa Mungu ana thamani kubwa. Kuokolewa kwa mtu ni kwa neema ya Mungu. Ni bure. Ila kwa fundisho la leo Yesu anasisitiza kwamba kwa namna nyingine kuna gharama kuingia Mbinguni. Maana mtu akiwa ameshampokea Yesu, ni lazima Yesu awe Bwana wa maisha yake. Asiwepo mtu na kisiwepo kitu chenye umuhimu kuliko Yesu na neno lake. Ndivyo Yesu anavyoonya akisema, Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu (m.26-27). Basi, kadhalika kila mmojawenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawe kuwa mwanafunzi wangu (m.33).

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz