Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 13 YA 31

Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze (m.24). Lakini, je, wokovu si kwa ajili ya wote? Ndiyo! Kwa nini, basi, wengine hawawezi kuingia? Dhambi zao ni kubwa mno? Hapana, si kwamba hawapokelewi au hawawezi kusamehewa dhambi zao. Sababu ni ugumu wa mioyo yao. Hawataki kutubu. Hawataki kumwambia Yesu dhambi zao na kumkabidhi maisha yao. Tafadhali ndugu, jitahidi! Omba umpate Roho Mtakatifu, ukikumbuka neno la Yesu, Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao (11:13)? Bila Roho hupati kumjua Yesu.

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz