Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Yesu analinganisha Ufalme wa Mungu na vitu vidogo sana, kama punje ya haradali (m.18-21), lakini ndani yake kuna nguvu sana inayotenda kazi kubwa! Inawezekana kwamba kazi ya Yesu machoni pa Wayahudi wengi ni ndogo na dhaifu maana wao walitegemea Masihi atawashinda adui zao Warumi na kuwafanya Waisraeli wawe watawala wa dunia nzima. Hata hivyo kazi ya Yesu ina nguvu sana na itaenea kwa ulimwengu mzima. Kwa hiyo watu toka pande zote za dunia wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu (m.29). Hii inatutia moyo sisi watumishi wa Bwana leo! Tutende kazi kwa uaminifu na ujasiri. Mungu yu pamoja nasi! Tafakari ilivyoelezwa katika 1 Kor 3:5-9, Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz