Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Yesu anazidi kwa mifano mingine kuwaonya sana Wayahudi - na sisi pia! Wayahudi walijadili sana kama kuna uhusiano kati ya ajali na dhambi. Hilo Yesu analikataa. Matukio kama hayo ni onyo kwetu ambao bado tunaishi hapa duniani. Tutubu, maana hukumu ya Mungu ya milele ni kali mno ukilinganisha na mateso ya Wagalilaya hao. Yesu anatusihi tutubu maana hukumu ya Mungu ya milele ni kali mno ukilinganisha na mateso ya watu hao. Maelezo machache kwa m.6-9: ‘Mtini’ ni Wayahudi. ‘Miaka mitatu’ ni muda Yesu aliokaa nao. ‘Usipozaa, ndipo uukate’ ni hukumu ya Mungu juu ya Wayahudi mwaka 70 BK walipoangamizwa na Warumi. Hata Tanzania jina la Yesu limetukuzwa sana! Je, umempokea?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz