Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 7 YA 31

Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo (m.15). Mfano wa Yesu unamhusu mtu ambaye kwa bidii yake mwenyewe amefanikiwa kupata mali nyingi. Huenda unafanana naye, ndugu msomaji? Katika hali kama hii unajaribiwa. Badala ya kumshukuru Mungu huenda unaanza kujivunia uwezo wako na kumsahau Mungu. Tena unaona ni haki kuifanyia mali yako utakavyo maana umeipata kwa nguvu yako. Somo lasema: Mpumbavu wewe! Uzima wako umetoka wapi? Mali yako itakusaidia katika hukumu ya Mungu?

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz