Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli (m.18). ‘Beelzebuli’ kwa jina jingine ni Shetani au Ibilisi. Yesu husisitiza kwamba Shetani hawezi kumtoa Shetani maana hataki kujiharibu mwenyewe. Watanzania wengi hufikiri kwamba waganga wa kienyeji wanaweza kuwaponya watu wenye mapepo. Lakini si kweli. Maana wao nao katika kazi yao hutumia nguvu ya Shetani. Wanatambua madai ya mapepo na wanajaribu kupunguza usumbufu wao kwa dawa fulani k.m. ubani. Ila kuwatoa hawawezi. Bali Yesu anaweza! Kumbuka anavyosema, Ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang'anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake (m.20-22). Umkimbilie Yesu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz