Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Kwa mifano yake Yesu anataka kutupa msukumo wa kuomba kwa ujasiri na bila kuchoka. Yesu ametupa haki ya kumwita Mungu kwa neno ‘Baba’, kwa maana wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake (Yn 1:12). Na Mungu ni baba mkamilifu. Katika m.9 Yesu ametupa ahadi kuhusu maombi, akisema, Ombeni, nanyi mtapewa. Na ili tusiwe na mashaka anairudia tena katika m.10 akisema, Kila aombaye hupokea! Yaani si utani. Kuna mambo kweli yatatendeka tukiitumia ahadi yake. Na tukiacha kuitumia, tukiacha kuomba, tutakosa baraka alizokusudia kutupa katika maisha yetu na katika usharika wetu. Na tusiombe mambo ya kimwili tu, lakini zaidi sana tuombe baraka za kiroho kama ilivyo katika ahadi yake anaposema, Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? (m.13)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz