Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano
Laiti mimi ningewekwa kuwa mwamuzi katika nchi hii, ili kila mtu mwenye neno au daawa aje kwangu, nimpatie haki yake (m.4; daawa = madai)! Absalomu alikuwa na uwezo sana wa kuamua kesi za watu. Lakini alikosa unyenyekevu. Kusudi lake sasa linaeleweka wazi. Anataka awe mfalme! Alijiona kuwa yeye anafaa zaidi kuliko baba yake. Wala hakuuliza Mungu anataka nini. Hakwenda Hebroni ili kuabudu, bali alitumia udanganyifu ili kufikia lengo lake la kuwa mfalme. Rudia m.7-10 ukizingatia jinsi Absalomu alivyotumia vibaya jina la Bwana ili kufanikiwa: Hata ikawa mwisho wa miaka minne, Absalomu akamwambia mfalme Tafadhali uniache niende nikaondoe nadhiri yangu, niliyomwekea Bwana huko Hebroni. Maana mimi mtumishi wako naliweka nadhiri hapo nilipokuwa nikikaa Geshuri katika Shamu, nikasema, Kama Bwana akinirudisha Yerusalemu kweli, ndipo nitamtumikia Bwana. Naye mfalme akamwambia, Enenda na amani. Basi akaondoka, akaenda Hebroni. Lakini Absalomu akapeleka wapelelezi katika kabila zote za Israeli kusema, Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta, ndipo mtakaposema Absalomu anamilikl huko Hebroni. Je, msomaji, unafanana naye?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/