Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano
Mwacheni alaani, kwa sababu Bwana ndiye aliyemwagiza. Labda Bwana atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye Bwana atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo (m.11-12). Daudi ananyenyekea mbele ya Mungu. Hajajaa hasira. Anakumbuka neno la nabii (12:10-11, Upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako. Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili) na kukubali adhabu ya Bwana. Hajilipii kisasi (kama Yesu - yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki; 1 Pet 2:23). Daudi ameshatubu dhambi yake na kutangaziwa msamaha. Kwa hiyo pamoja na adhabu anaitumainia na kung’ang’ania neema ya Bwana. Siku hizo Daudi alitunga Zaburi 3 na 63 ambazo unaweza kuzisoma ukiwa na nafasi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/