Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 7 YA 31

Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda (m.30). Katika hili Daudi ni mfano wa Yesu ambaye anaitwa mwana wa Daudi. Daudi alisalitiwa na Absalomu na Ahithofeli (m.31, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu). Yesu alisalitiwa na Yuda Iskariote. Daudi alivuka kijito cha Kidroni (m.23, Mfalme mwenyewe naye akavuka kile kijito Kidroni). Yesu naye alivuka hapo pamoja na wanafunzi wake usiku ule wa mwisho (Yn 18:1, Yesu alitoka pamona na wanafunzi wake kwenda ng’ambo ya kijito Kedroni, palipokuwapo bustani). Daudi alikuwa anafadhaika na kulia kwenye mlima wa Mizeituni (m.30, Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda). Yesu alifanya vilevile: Kisha wakaja mpaka bustani iitwayo Gethsemane; Yesu akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa muda niombapo. Akamtwaa Petro na Yakobo na Yohana pamoja naye, akaanza kufadhaika sana na kuhangaika. Akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe (Mk 14:32-34). Yesu aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini (Lk 22:39-44). 

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/