Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 31 YA 31

Shabaha kuu ya mapigo na maangamizi ni kuwaonya watu ili yamkini watubu dhambi na uasi wao. Lakini watu hawataki kuungama. Wanaendelea kuwa wagumu. Ugumu wao unawaunganisha na malaika waovu walioanguka toka utukufu wa Mungu. Hawa hawana nguvu tena. Dhambi humwingia mtu polepole. Majaribu ya leo yasipodhibitiwa, kesho huwa dhambi, kama alivyofafanua Yakobo: Ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti (Yak 1:15). Kubali kuwepo kwa dhambi na uovu wako, uone haja ya kutubu dhambi zako mbele za Mungu wako.

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/