Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 1 YA 31

Je, umejisikia kuwa mtu aliyesahauliwa na Mungu? Basi, bila shaka unajisikia nyumbani ukisoma kilio hiki cha Daudi. Katika m.3 lipo ombi zuri wakati mioyo yetu inafadhaika, Ee BWANA, ... uyatie nuru macho yangu. Hivyo tu tutapewa kuona ukweli wa ushuhuda wa Daudi kwamba yupo Mungu anayetusaidia wakati wa mateso ili tuweze kufanya kama Daudi, akisema, Nami nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako. Naam, nimwimbie Bwana, Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu (m.5-6). Jaribu kukumbuka Mungu alivyomtendea Daudi kwa ukarimu. Je, hajawahi kukutendea vivyo hivyo? Basi, uendelee kuzitumaini fadhili za Mungu, nao moyo wako utaufurahia wokovu wake.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/