Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 6 YA 31

Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye Yerusalemu, Ondokeni, tukakimbie (m.14). Daudi alikuwa ni hodari sana wa vita. Sasa uhodari wake uko wapi? Mbona anakimbia? Nafikiri kuna sababu nne. 1. Hakutaka kupigana vita na mwana wake mwenyewe (m.14, Fanyeni haraka, tuondoke, Absalomu asitupate kwa upesi, na kutuletea maovu). 2. Walioshikamana na Absalomu ni wengi kuliko wa kwake (m.13, Mioyo ya watu wa Israeli inashikamana na Absalomu). 3. Hakutaka Yerusalemu uharibiwe. Mji huu ndio uliowafanya Waisraeli wawe kitu kimoja (m.14, Absalomu asiupige mji huu kwa makali ya upanga. Pia katika m.25 Daudi anafikiria mji akimwambia Sadoki, Rudisha sanduku la Mungu mjini). 4. Hakuwa na uhakika kama Bwana yu upande wake. Bila shaka anakumbuka neno la Mungu kwake katika 12:10, Upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako. 15:25-26 inaonyesha kwamba ingawa Daudi hana uhakika, anaendelea tu kujiweka mikononi mwa Bwana, Nikipata kibali machoni pa Bwana atanirudisha, na kunionyesha tena sanduku hili, na maskani yake.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/