Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 10 YA 31

Ahithofeli alikuwa ni mtu wa hekima. Alimsaidia sana Daudi katika utawala wake (k.m. katika 15:12 anaitwa mshauri wake Daudi, na 16:23 inasema, Shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi). Kwa hiyo alikuwa na mamlaka kubwa. Ndipo akaanza kuipenda hiyo mamlaka kuliko kuupenda utii na ukweli. Kwa hiyo alipoona kuwa Absalomu ana nguvu kuliko Daudi akajiunga naye. Shauri lake la kwanza tuliona jana. Shauri lake la pili pia lilikuwa jema kwa upande wa Absalomu, imeandikwa katika m.14b. Ahithofeli alijua kuwa lisipofuatwa, Daudi atashinda. Lakini angalia pia hapo kwamba Bwana alikuwa amekusudia kulivunja shauri jema la Ahithofeli, ili Bwana alete mabaya juu ya Absalomu. Na Bwana akazuia lisifuatwe ili Daudi apewe haki. Daudi mwenyewe aliomba hivyo katika 15:31, Daudi akasema, Ee Bwana, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili.

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/