Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano
Farasi wanawakilisha hukumu ya Mungu dhidi ya dhambi na uasi wa mwanadamu. Farasi wale namba 2, 3 na 4 ni dhiki, vita duniani na ughali wa chakula. Matokeo yake ni njaa na vifo. Namba 1 inaweza kuleta picha juu ya Yesu (ukipenda, unaweza kulinganisha m.2 na Ufu 19:11-16). Ila pengine sivyo, maana Yesu ndiye anayefungua muhuri huu (m.1). Na tukilinganisha na Lk 21:8-11, Yesu anafundisha juu ya mambo hayohayo, naye anataja vita, njaa na masiha wa uongo. Kuna waongo wanaodai kuwa wao ni Kristo na kujaribu kufanana naye. Jiepushe nao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/