Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Mfalme akamwambia, Kwa nini aende nawe? Lakini Absalomu akamsihi sana, naye akamwacha Amnoni na wana wote wa mfalme waende naye (m.27). Daudi alisitasita. Huenda alihisi kwamba Absalomu alitaka kufanya uovu, maana chuki yake kwa Amnoni alishindwa kuificha. Kama Yonadabu alivyomwambia Daudi, Asidhani bwana wangu ya kwamba wamewaua vijana wote, wana wa mfalme; maana ndiye Amnoni peke yake aliyekufa; yakini haya yamekusudiwa kwa kinywa chake Absalomu tangu siku ile alipotenzwa nguvu umbu lake, Tamari (m.32). Hata hivyo Daudi akamruhusu. Alikosa msimamo. Tunaona tena kwamba nguvu na ujasiri wa Daudi wa kuwasimamia wana wake ulipungua sana. Na hayo ni kutokana na lile tendo baya alilokuwa amefanya mwenyewe. Dhambi hutoa matunda mabaya!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/