Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Akamtenza nguvu, akalala naye (m.14). Ina maana ya kwamba Amnoni alimlazimisha Tamari kujamiiana naye. Tamari alikuwa amemwambia ukweli: Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli (m.13). Tutafute wapi sababu ya tendo hili baya? Sababu moja ni jinsi Amnoni alivyomtamani Tamari. Hata akawa kama kipofu. Sababu nyingine ni Amnoni kuwa na rafiki mwenye maadili mabaya. Badala ya kumwonya, alimsaidia kufanya dhambi. Tukio hili lituonye na sisi!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/