Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Dalili za Daudi kusamehewa zilikuwepo. 1. Hakufa. 2. Alikubaliwa na Mungu kuendelea kuwa mfalme. 3. Aliendelea kushinda juu ya adui zake (m.29, Daudi akawakusanya watu wote akaenda Raba, akapigana nao, akautwaa). 4. Alipata tena mwana mwingine na Bath-sheba (m.24, Daudi akamfariji Bath-sheba mkewe, akaingia kwake, akalala naye; naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sulemani. Naye Bwana akampenda). Ila tendo baya la Daudi liliwapa adui wa Bwana nafasi kubwa ya kukufuru. Kwa sababu hiyo, na ili Daudi aelewe vizuri, Bwana pia alimpa Daudi adhabu ili iwe wazi kwamba kufanya dhambi ni hatari! 1. Vita ndani ya nyumba yake. 2. Wake zake watabakwa. 3. Yule mtoto wa uzinzi atakufa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/