Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Hasira ya Daudi iliwaka sana juu ya mtu yule asijue kwamba mfano huu unamhusu yeye mwenyewe! Astahili kufa (m.5). Ndipo Nathani akaanza kusema naye wazi wazi, Wewe ndiwe mtu huyo (m.7). Kwa nini umelidharau neno la Bwana ... umenidharau (m.9-10). Hapa tunaona kwamba kulidharau Neno la Mungu ni kumdharau Mungu mwenyewe. Daudi alikuwa ameua, amezini, ameiba, amemshuhudia jirani yake uongo na amemtamani mke wa jirani yake (yaani, amri ya 5 hadi amri ya 10). Yote haya kwa wakati mmoja!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/