Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

SIKU 24 YA 30

Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza Bwana (m.27). Daudi alijitahidi kwa nguvu sana kuificha dhambi yake isijulikane. Lakini ujanja wake hazikufanikiwa kwanza (m.13, Daudi akamwalika [Uria], akala, akanywa mbele yake; naye akamlevya; hata wakati wa jioni akatoka kwenda kulala kitandani mwake pamoja na watumishi wa bwana wake, lakini hakushuka nyumbani kwake). Kisha Daudi akaamua kutumia nguvu na mamlaka zake za kiufalme ili Uria apate kuuawa, akafanikiwa. Dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti (Yak 1:15). Siku zake saba za maombolezo zilipokuwa zimekwisha, ndipo mke wa marehemu akachukuliwa na Daudi akawa mke wake. Lakini mbele ya Mungu dhambi i wazi, haifichiki! Hali yetu ya kweli kama ilivyoelezwa katika Ebr 4:13, Hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake [Mungu], lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/