Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

SIKU 26 YA 30

Nimemfanyia Bwana dhambi (m.13). Hapo tunaona tofauti kati ya Daudi na Sauli. Daudi alikuwa anaishi maisha yake mbele ya Bwana. Alikuwa anampenda Bwana, lakini sasa alikuwa amemchukiza. Kwa hiyo Daudi akaona uchungu (wakati wa matukio haya alitunga Zab 51. Katika m.1-9 unaweza kusoma anavyoeleza uchungu wake). Bali Sauli alipoambiwa dhambi zake, hakuonyesha uchungu kama huu. Alisema tu: "Nimefanya dhambi". Tena alijitetea (1 Sam 15:24-26, Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya Bwana, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu Bwana. Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la Bwana, Bwana naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli). Kati ya hawa wawili, Daudi tu ndiye aliyesamehewa kabisa na Mungu: Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana dhambi. Nathani akamwambia Daudi, Bwana naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa (m.13). Mit 28:13 hutoa sababu: Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema. Katika Zab 32:1-5 unaweza kusoma jinsi Daudi mwenyewe alivyoelewa jambo hili baada ya Mungu kumfundisha.

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/