Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Mfalme Daudi alikasirika sana alipopata habari - lakini hakutenda lo lote! Kufuatana na sheria ya Musa, Amnoni amelaaniwa kwa sababu ya tendo lake! Alitakiwa kuuawa (Law 20:17, Mtu mume akimwoa umbu lake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mume; ni jambo la aibu; watakatiliwa mbali mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa umbu lake; naye atauchukua uovu wake. Kum 27:22, Alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye). Labda Daudi alikosa msimamo kwa sababu ya kule kuanguka kwake mwenyewe katika dhambi kama iyo hiyo. Ila kwa njia hiyo alizidi kuikaribisha vita ndani ya nyumba yake, kama nabii alivyosema, akimwambia Daudi neno la Mungu, Sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako (12:10)! Maana chuki ya Absalomu iliwaka kwa nguvu alipoona kuwa baba yake hakumpa Amnoni adhabu: Absalomu hakusema na Amnoni wala kwa heri wala kwa shari; kwa maana Absalomu alimchukia Amnoni kwa kumtenza nguvu umbu lake Tamari (m.22)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/