Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Laodikia ulikuwa mji tajiri, wenye viwanda. Ulitegemea maji moto kutoka mlimani. Lakini yalibadilika njiani. Yakifika mjini yalikuwa vuguvugu. Tabia ya Wakristo wa mji huu ilifuata hali ya maji hayo. Je, imani yako kwa Kristo ni ya aina gani? Ni baridi, moto au vuguvugu? Uvuguvugu wa imani unatokana na tabia ya kujitosheleza. Yesu anadhihirisha hiyo katika m.17, Wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Mwombe Kristo alete moto uamshe imani yako, ili maisha yako yawe mali yake. Usijivune, wala usirudishwe nyuma na mafanikio yako. Uamue kuwa mali ya Kristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/