Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

SIKU 21 YA 30

Ufunguo wa Daudi unawakilisha mamlaka ya Kristo ya kufungua mlango wa kuingia katika ufalme wake. Mlango wa Kristo umefunguliwa tayari. Hakuna awezaye kuufunga. Ukiingia kwa Kristo unalindwa. Pia anakufungulia mlango wa utumishi. Wale wapinzani ambao awali walidharau Wakristo, Yesu atawafanya wawageukie Wakristo kutafuta msaada wa kiroho: Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda (2:9). Halitokani na nguvu za Wakristo, maana nguvu zao ni chache (m.8,  Unazo nguvu kidogo). Hiyo ni faraja kwetu tunapojikuta hatuna nguvu. Kristo anawategemeza watumishi wake.

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/