Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

SIKU 20 YA 30

Kanisa la Sardi lilikabiliwa na kifo cha kiroho. Likikosa mwamko wa kiroho likakengeuka, likawa tofauti na lilivyopokea hapo mwanzo. Hivyo ule uhai wa ndani ulififia, likabaki na matendo fulani ya nje tu yaliyowadanganya watu. Ila Yesu hadanganyiki. Huona kanisa lilivyochafuka. Kwa hiyo Yesu analionya, Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako (m.3). Kanisa linaitwa lirudi katika ukweli wa Kristo. Bila kumrudia Mungu hakuna kutambuliwa naye. Kutambuliwa na Mungu ni kuandikwa kitabuni mwake. Unapenda kutambuliwa na Kristo? Tubu dhambi zako na kumwamini Yesu.

Andiko

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/