Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Mji wa Thiatra ulijaa vituo vingi vya biashara na ufinyanzi. Kanisa la huko linasifiwa kwa upendo, subira na matendo mema. Tukue katika upendo, imani na matendo ya huduma. Yezebeli alimdanganya mfalme Ahabu (1 Fal 21). Huyu mwanamke alishakufa zamani, yaani Yohana anamtumia kama mfano tu wa mtu fulani aliyesumbua huku Thiatira. Kuzini ni kukosa uaminifu. Yezebeli hakutubu na kubadilika. Mungu anakupa wewe leo wasaa wa kutubu. Mfuate Kristo. Nuru yake unaangamiza uovu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/