Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 15 YA 15

Tofauti na upendo wa mwanadamu, ambao siku zote ni wa kigeugeu na wamuda, upendo wa Mungu haushindwi, hata iweje.

Naipenda Zaburi 136. Napenda Zaburi zote, lakini siku zote inanifurahisha kila ninapoisoma. Napenda marudio yanayoifanya Zaburi hii kuwa bora kuliko zote. Naipenda kwa sababu Zaburi 136 ni Zaburi ya historia ambayo, kwa sababu ya kujizuia kwake, inageuka kuwa Zaburi ya upendo. Naipenda kwa sababu mara kwa mara inasisitiza kile waliokata tamaa wanataka kukisikia tena na tena-- si mara moja au mara mbili, bali mara ishirini na sita! Sasa, nadhani kila Mungu anapozungumza, wewe na mimi kwa unyenyekevu tunatakiwa kunyamaza na kusikiliza, lakini pia nadhani tunahitaji kusikiliza kwa makini kwenye maeneo ambayo Mungu anapenda kuyarudia, na hasa anapojirudia mwenyewe mara nyingi!

Kwa nini Mungu anarudia rudia, tena na tena katika kalamu ya mtunga Zaburi, "kwa maana fadhili zake ni za milele"? Kuna majibu mawili kwa swali hili.

Kwanza, hakuna ukweli imara na wenye misingi ya mtazamo wa ulimwengu na wenye utambulisho binafsi kibiblia kuliko huu. Hadithi ya kibiblia ni ipi? Ni habari ya Mungu wa upendo akiujia ulimwengu katika utu wa mwanaye wa upendo kuanzisha ufalme wake wa upendo kwa dhabihu imara ya upendo, kutusamehe kwa upendo na kutuvuta katika familia yake ya upendo, na kututuma kama mabalozi wa upendo uleule. Tumaini zima la mwanadamu aliyeanguka limekaa katika jambo hili moja--kwamba kuna Mwokozi ambaye kwa upendo wa milele anakomboa, anasamehe, anapatanisha, anabadirisha, na anatoa upendo. Pasipo hivyo, Biblia ni kitabu cha hadithi tamu na kanuni za kusaidia, lakini hakina nguvu ya kurekebisha kile ambacho dhambi imekivunja.

Sababu ya pili kwa Mungu anarudia rudia ni kwa sababu hatuna uzoefu wa upendo wa namna hii katika maisha yetu. Siku zote unaanza kuelewa kitu kipya kwako kutokana na hatua katika uzoefu wako. Upendo wote wa kibinadamu ambao tumeuona umekuwa na unafiki kwa namna fulani. Lakini si upendo wa Mungu; upendo wake ni mkamilifu na mkamilifu daima. Ni ukweli pekee wa ajabu kwa maisha ya mwamini. Mungu ameweka upendo wake kwetu na hatauondoa tena kamwe. Kuna sababu ya kuendelea, pasipokujali ugumu wa maisha na jinsi unavyojisikia dhaifu. 

Learn more  about New Morning Mercies: A Daily Gospel Devotional by Paul David Tripp.

Andiko

siku 14

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/