Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 13 YA 15

Ndiyo, ni kweli--Mungu atabaki kuwa mwaminifu hata kama wewe hutakuwa mwaminifu, kwa sababu uaminifu wake uko juu ya vile alivyo, siyo kwa kile unachofanya.

2 Tomotheo 2:13: "Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa--kwa maana hawezi kujikana mwenyewe." Mstari huu unatuonesha njia tofauti ya kuishi, kitu ambacho wengi wetu hatuna. Wanadamu wengi wanaamini kuwa " maisha yako mikononi mwako"," unatengeneza ama kuharibu maisha yako," "lipa pesa yako na uchukue unachotaka," " hakuna wa kumwangalia au kumlaumu kwa jinsi ulivyo isipokuwa mwenyewe". Kwa mtazamo huu, wewe ndiye mwenye kuamua mstakabali wako. Huna cha kutegemea zaidi ya hisia zako, nguvu zako, hekima yako, uwezo wako wa kutarajia yanayokuja, tabia na ukomavu wako, na karama ulizopewa. Inatisha "wewe kushindana" na maisha ya dunia.

Lakini kukaribishwa katika familia ya Mungu kunapindua vyote hivi. Mungu hakusamehi tuu dhambi zako na kukuhakikishia kiti katika umilele, lakini pia katika maisha mapya. Haya maisha mapya siyo tu kutii kufuata mfumo wa tabia ya Mungu. Hapana, ni kuhusu Mungu mwenyewe kuhakikisha kuwa mwaminifu kwako milele, akiachilia hekima yake, nguvu, na neema kwa ajili yako milele. Hebu fikiria. Yeye aliyeumba na kutawala dunia, yeye ambaye ndiye kielelezo halisi cha kupenda, kweli, na wema, na yeye pekee mwenye nguvu ya kshinda dhambi amekuchagua, kwa sababu ya neema yake, kukukumbatia kwa mikono yake ya upendo mwaminifu na kukukinda, na hatakuacha.

Unaweza kuondoa maisha yako mikononi mwako kwa sababu Mungu ameyaweka mikononi mwake. Hii haimaanishi haijalishi unaishije, lakini kwamba usalama wako uko haupatikani katika uaminifu wako, bali uaminifu wake. Aweza kuaminiwa hata usipoamini. Atafanya lilio jema na bora hata kama wewe hufanyi. Na yeye ni mwaminifu kukusamehe wakati neema ya mashitaka inaonesha jinsi ambavyo hujawa mwaminifu.

kuliko kukupa wewe leseni ya kufanya chochote, kweli hii ikupe hamasa ya kuendelea. Neema yake inakuita wewe kuwekeza katika jambo moja ambalo halitakuangusha, na hilo jambo moja ni uaminifu wa Bwana wako.

siku 12siku 14

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/