Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano
Kwa mwamini, hofu siku zote ni kumsahau Mungu. Kama Mungu ni muweza, na mamlaka yake ni kamili, hekima, haki na wema, kwa nini uwe na hofu?
Maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda, ni dhahiri kama yalivyokuwa karne na karne zilizopita yaliposemwa kwa mara ya kwanza. Yuda livamiwa na majeshi yenye nguvu ya Mfalme wa Ashuru, Senakeribu. Hezekia aliwaanda na kuwapa silaha Yuda tayari kwa vita, lakini hakufanya hivyo tuu. Aliwakusanya watu na kuzungumza nao juu ya jambo hili muhimu. Alijua kwamba nyakati kama hizi watu wa Mungu huingiwa na hofu, na alijua hiyo hofu inatoka wapi. Mara nyingi nyakati hizi za changamoto watu wa Mungu huchanganyikiwa kwa sababu husahau utambulisho wao. Hujisahau kama wao ni nani kama watoto wa Mungu na kusahau Mungu katika ukuu wake na utukufu. Kwa hiyo wakati huo, Hezekia alijua kwamba hawezi tuu kuwa mfalme mzuri na jemedari hodari; lazima pia awe Mchungaji mwenye hekima kwa watu wake.
Walipokuwa wanajiandaa na uvamizi wa Waashuru, Hezekia hakutaka watu Yuda wafikirie ujasiri wao, uzoefu wao wa vita, na weledi wao kutumia silaha. Alitaka wajue kwamba wamebarikiwa ajabu na jambo lingine, ambalo hawawezi kulisahau. Kwa hiyo alisema: "Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote waliyo pamoja naye....kwake upo mkono wa mwili, ila kwetu yupo Bwana, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu" ) 2 Nyakati 32: 7-8).
kutakuwa na wakati ambapo utauliza, " ujasiri uko wapi wa kukabili hali ninayopitia?" Hezekia anakupa jibu: Tazama mbinguni na mkumbuke Mungu wako." Kama mwana wa Mungu, huwezi kuachwa upigane mwenyewe.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.
More