Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 8 YA 15

Mungu anakutaka uamini ndipo akutengeneze kuwa mtu ambaye hakika anaishi kwa imani.

Sijui umekifikiria kiasi gani hili, lakini imani si kitu cha asili kwa ajili yako ama yangu. Mashaka ni kitu cha asili. Hofu ni kitu cha asili. Kuishi kwa uzoefu ni kitu cha asili. Kufikiria " itakuwaje" akilini mwako kabla ya kwenda kulala au unapoamka asubuhi ni kitu cha asili. Kuishi kulingana na mawazo ya akili yako na jinsi mwili unavyohisi ni kitu cha asili. Kuonea wivu maisha ya mtu mwingine na kufikiria kwa nini hukuwa wewe ni jambo la asili. Kutamani kwamba ungekuwa unatawala watu, hali na mahali unapotaka kuwa ni jambo la asili. Kudanganya kama njia ya kutaka kupata kutawala na kupata unachotaka, ni jambo la asili. Kutafuta amani mahali ambapo huwezi kuipata ni kitu cha asili. Kuwa na shauku ya kubadi mambo ambayo una uwezo wa kuyabadili ni jambo la asili. Kutoa nafasi ya kujihurumia, kukata tamaa, kuwa na msongo wa mawazo, au kushindwa, ni jambo la asili. Kujishughulisha na mambo mengi, vitu mbalimbali, chakula, au vitu vingine ni jambo la asili. Kushusha kiwango chako ili kukabiliana na kuvunjika moyo ni jambo la asili. Lakini imani si jambo la asili kwetu.

Kwa hiyo, katika neema, Mungu anatupa kuamini. Kama Paulo anavyosema katika Epheso 2: 8, imani ni karama ya Mungu. Hakuna tena ufahamu unaopingana na kawaida, mwanadamu aliye haribiwa na dhambi kuliko imani katika Mungu. Hakika, tutaweka imani yetu katika vitu vingi, lakini siyo katika Mungu ambaye hatuwezi kumwona au kumsikia, ambaye anafanya ahadi kubwa zinazoonekana haziwezekani kuzitimiza. Mungu hutupa kwanza nguvu ya kuamini, lakini haishii hapo. Kwa neema hutenda kazi katika mazingira, maeneo, na maisha yetu ya kila siku kututengeneza, kutuponda, kutukunja, na kutuumba kuwa watu wanaojenga maisha katika ukweli kwamba anaishi na huwapa thawabu wale wamtafutao ( Waebrania 11: 6).

Wakati mwingine ukikabiliwa na yasiyotarajiwa, wakati mgumu ambao usingependa kuupitia, kumbuka kwamba wakati kama huo hauonyeshi kwamba Mungu amekusahau, bali yeye aliye karibu sana na wewe na anatenda mema. Anakuokoa na mawazo kwamba unaweza kuishi maisha uliyokusudiwa kuishi ukiwa unategemea rasilimali zisizotosha za hekima yako, na nguvu zako, na anakubadilisha kuwa mtu anayeishi maisha yanayoongozwa na imani iliyosimama ndani ya Mungu. Yeye ndiyo mwisho wa ufinyanzi, na sisi ni udongo wake. Hatatuondoa katika gutudumu lake la ufinyanzi mpaka vidole vyake vimetufinyanga kuwa watu tunaoamini na hatuwi na mashaka.

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/