Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 11 YA 15

Kama umewekwa huru katika kutafuta mafanikio ili ujisikie vizuri kuhusu wewe, unajua neema imekutembelea.

Ni juhudi kubwa za kibinadamu. Ni kitu ambacho sisi wote tunakitaka. Wote tunapenda kujisikia vizuri. Tunapenda kujisikia kwamba tuko sawa. Ni matakwa ambayo yanatisha na kutuhangaisha ambayo ni neema tu inaweza kutuweka huru.

Hiki ndicho kinatokea kwetu wote--tunatafuta pumziko kwingine wakati linapatikana kwingine, na hatufanikiwi. Kuwategemea wengine kwa ajili ya ustawi wako hakusaidii. Kwanza, huwezi kuwa mwema, huwezi kudumu, kupata sifa unazotaka kutoka kwa wanaokuzunguka. Utaharibu tuu. Utakatisha tamaa tuu. utakuwa na siku mbaya. Utapoteza mwelekeo. Nyakati zingine, utasema au kufanya vitu ambavyo hukupaswa kufanya. Kwa kuongezea ukweli huu kwamba watu wanaokuzunguka hawako tayari kuchukua mzigo wa kuwa Masihi wako. Hawataki kuishi na wajibu wa kuwa na utambulisho wako mikononi mwao. Kutegemea watu kwa ajili ya thamani yako hakusaidii.

Amani ambayo mafanikio yanatoa haiaminiki pia. Kwa sababu wewe si mkamilifu, mafanikio yoyote utakayopata ghafla yatafuatiwa na kushindwa kwa namna fulani. Ndipo unapokuja ukweli kwamba furaha ya mafanikio ni ya kitambo tuu. Haichukui muda kabla hujaanza kutafuta mafanikio mengine ili kukufanya uendelee mbele. Ndiyo maana ukweli kwamba Yesu amefanyika haki yetu ni wa thamani sana. Neema yake imetuweka huru milele na hitaji la kuthibitisha haki na thamani yetu. Kwa hiyo tunajikumbusha kila siku tusitafute kwingine kitu ambacho tayari tumekwisha pewa. " Na kazi ya haki itakuwa amani, na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima" ( Isaya 32: 17). Haki hiyo inapatikana ndani ya Kristo pekee.

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/