Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 14 YA 15

Usikate tamaa leo. Unaweza kuachana na maswali ya "itakuwaje" na " isipokuwa tuu" mikononi mwa anayekupenda na anatawala vitu vyote.

Ijapokuwa wewe ni mtu wa imani ambaye amepata kiwango fulani cha ufahamu wa Biblia na elimu ya theologia, kuna jambO moja ambalo unaweza kuwa na uhakika nalo--Mungu atakuchanganya. Theologia yako itakupa mipaka ya ufafanuzi wa uzoefu wako. Amri, kanuni na mifano ya maandiko vitakufikisha tuu katika kufikiria juu ya maisha yako. Kutakuwa na nyakati ambapo utakuwa hujui hasa nini kinaendelea. Kusema ukweli, utakabiliwa na nyakati ambapo kile ambacho Mungu amesema kitu chema katika maisha yako hakitaonekana chema. Chaweza kuonekana kibaya, kibaya sana. 

Sasa, kama imani yako imejengwa katika uwezo wako wa kuelewa yaliyopita, yaliyopo, na yajayo, basi nyakati za kuchanganyikiwa zitakuwa nyakati za kudhoofisha imani yako. Lakini ukweli ni kwamba unakuwa hujapewa uchaguzi wa aina mbili tu—elewa kila kitu na upumzike kwa amani or elewa kidogo na uteseke na wasiwasi. Kuna njia ya tatu. Ni njia ya kweli ya kibiblia. Biblia inakuambia kwamba amani ya kweli inapatikana katika kutulia katika hekima ya yeye ashikaye " itakuwaje" na "isipokuwa tuu" katika mikono yake ya upendo. Isaya ameliweka hili vizuri kwa maneno haya ya faraja: " Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea, kwa kuwa amekutumaini" ( Isaya 26:3).

Imani ya kweli, imara, ya kudumu, isiyopanda na kushuka kutokana na mazingira, haitakiwi kuonekana katika kuyagawanya maisha yako mpaka utakapoelewa vipengele vyote. Hutaielewa yote kwa sababu Mungu, kwa ajili yako na utukufu wake, huweka katika mazingira ya usiri. Kwa hiyo imani inapatika tuu katika kuamini, kumwamini yeye aliye katika uangalizi wa hali ya juu wa mambo yote yanayokuibia amani yako. Anajua, anaelewa, anatawala yote yanayoonekana ni machafuko, hastushwi, hachanganyikiwi, hana mashaka wala hakosi usingizi, hapumziki, hashughulishwi na jambo moja kiasi cha kutokujali lingine, na hana upendeleo.

Unahitaji kujikumbusha mara kwa mara juu ya hekima yake na upendo wake, si tu kwa sababu itafanya maisha yako yawe ya maana, ila kwa sababu itakupa pumziko na amani katika nyakati ambazo sisi sote tunakabiliana nazo nyakati fulani-- wakati maisha yanapoonekana hayana maana.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/