Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 10 YA 15

Kama umewekwa huru katika kutafuta mafanikio ili ujisikie vizuri kuhusu wewe, unajua neema imekutembelea.

Ni jitihada za kibinadamu. Ni shauku ambayo wote tunahangaikia. Wote tunapenda kujisikia vizuri. Wote tunataka kujiona tuko sawa. Ni shauku ya kutisha ambayo ni neema tuu inayoweza kutuweka huru.

Hiki ndicho kinachotokea kwetu wote--tunatafuta kupumzika katika njia ambayo haitusaidii. Kujilinganisha na wengine ili ujisikie vizuri haina maana. Kwanza, hutakuwa hutakuwa mwema sana, mwenye kudumu, ili kupata sifa za watu wengine unazozitafuta. Utaharibu tuu. Utakatisha tamaa. Utakuwa na siku mbaya. Utapoteza mwelekeo. Wakati fulani utafanya mambo ambayo hukupaswa kufanya. Na kwa hilo hata watunwanaokuzunguka hawako tayari kubeba mzigo wa wao kuwa Masihi wako. Hawataki kuishi wakiwa na wajibu wa kubeba utambulisho wako mikononi mwao. kutafuta watu ili uwe na kibali hakutakusaidia.

Amani ambayo mafanikio hutoa haiminiki pia. Kwa sababu wewe siyo mkamilifu, mafanikio yoyote utakayoweza kuyapata yatafuatiwa na kushindwa kwa namna fulani. Ndipo unakuja ukweli kwamba furaha ya mafanikio ni ya kitambo tuu. Haichukui muda kabla ya kuanza kutafuta mafanikio mengine ili uendelee. Ndiyo maana ukweli kwamba Yesu amekuwa haki yako ni wa thamani sana. Neema yake imetuweka huru milele katika kuthibitisha haki yetu na thamani yetu. Kwa hiyo tunajikumbusha kila siku kwamba tusitafute kitu ambacho tayari tumekwisha kupewa. "Na matokeo ya haki itakuwa amani, na matokeo ya haki, utulivu na tumaini milele" ( Isaya 32: 17). Na haki hiyo inapatikana ndani ya Kristo peke yake.

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/