Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 1 YA 15

Hapa ndiyo mstari wa mwisho. Maisha ya Kikristo, Kanisa, imani yetu si juu yetu, ni kuhusu Yeye-- Mipango yake, Ufalme wake, Utukufu wake.

Hakika ni mapambano juu ya mapambano. Ni kitu kilicho gizani kwetu sote. Ni kitu kinachovuruga maisha yetu na kuharibu uhusiano wetu. Ndicho kinachopotosha mawazo yetu na kuteka matamanio yetu. Ni kitu cha mwisho katika vitu vyote vinavyoweza kutusaidia katika shauku yetu ya neema. Ni vita ambayo hakuna anayeweza kuikwepa. Ni mahali ambapo watu kumi kati ya kumi kati yetu tunahitaji ukombozi. Ni vita ambayo Mungu anapigana kwa niaba yetu kutufanya tukumbuke kuwa maisha si juu yetu. Ni kuhusu Mungu --Mipango yake, Ufalme wake, na Utukufu wake. 

Hii ndiyo sababu kwa nini maneno matatu ya mwanzo wa Biblia ni maneno muhimu sana: " Hapo mwanzo, Mungu...." Haya ni maneno yenye nguvu sana. Yanabadilisha kila kitu, kutoka jinsi unavyofikiri mustakabali wako, maana, na kusudi la njia unayoitumia kukabiliana na hata na jambo dogo la kazi za mwanadamu. Kila kilichoumbwa kiliumbwa na Mungu na kwa ajili ya Mungu. Utukufu wote wa uumbaji wa Mungu uliumbwa kuelekeza kwenye utukufu wake. Mbingu ni za kwake, ziliumbwa kufanya kazi kulingana na kusudi na mpango wake. Hiyo ikijumuisha wewe na mimi. Hatujaumbwa kuishi maisha ya kujitegemea, maisha ya kujiongoza. Hatukukusudiwa kuishi kulingana na mipango yetu wenyewe, tukiishi kwa utukufu wetu wenyewe. Hapana, tuliumbwa kuishi kwa ajili yake. 

Ni wapi maisha haya ya kimungu yanatakiwa kuonekana? Yanatakiwa yaonekane si tuu katika misingi ya kidini katika maisha yetu, lakini katika kila nyanja ya uwepo wetu. Ninapenda jinsi Paulo anavyoeleza hili katika 1 Wakorintho 10: 31: " Basi mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu". Paulo anapofikiria juu ya wito wake wa kuishi kwa utukufu wa Mungu, hafikirii kwanza ukubwa, kubadili maisha, kujiangalia mwenyewe maisha ya kiroho. Hapana, anaona kama ni kitu cha kawaida na cha kujirudiarudia kama kula na kunywa. Hata maisha yangu ya kawaida, kazi zinazoonekana za muhimu katika maisha yangu lazima zifanywe na zielekezwe katika hamu ya utukufu wa Mungu. Sasa, sijui wewe, lakini katika maisha mara nyingi najisahaulisha uwepo wa Mungu , mbali na utukufu wakez!.

Hebu na tuanze mwaka mpya kwa kukiri kwamba hakuna kitu kisicho cha asili kwetu kuliko kuishi kwa utukufu wa mtu mwingine. Ukiri huu ni mlango wa kutokukata tamaa ila wa matumaini. Mungu alijua katika dhambi zako hutaweza kuishi hivi, ndiyo maana alimtuma mwanaye kuishi maisha ambayo wewe huwezi, na kufa kwa niaba yako, na kufufuka tena, akishinda dhambi na mauti. Alifanya hivyo si tu kwamba usamehewe kwa utii wako kwa utukufu wako, bali kuwa na kila neema unayoihitaji kuishi kwa ajili ya utukufu wake. Unapokiri uhitaji wako wa msaada, unajiunganisha na msaada wake aliouweka kupitia mwanaye, Yesu. Toka kwa matumaini kupata msaada wake leo.

Learn more  about New Morning Mercies: A Daily Gospel Devotional by Paul David Tripp.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/