Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano
Kama umilele ndiyo mpango, basi haina maana kukata tamaa kwa mahitaji yako haya ya muda mfupi.
Hakuna mashaka juu ya hilo-- Biblia ni kitabu cha picha kubwa ambacho kinatutaka nasi tuishi maisha ya picha kubwa. Kinatanua mawazo yako kwa sababu inakutaka ufikirie mambo kabla ulimwengu haujaumbwa na miaka elfu moja katika milele. Biblia haiukuruhusu kuishi kwa kitambo tuu. Haiukupi nafasi ya mawazo yako, mapenzi yako, maneno yako, na matendo yako kuwa madogo wakati wowote. Kuna wakati, hisia zako zaweza kuonekana muhimu kuliko zilivyo halisi. Kuna wakati, mahitaji yako yanaweza kuonekana muhimu zaidi kuliko ukweli halisi. Tunatakiwa tuishi maisha ambayo yameunganishwa na mianzo na miisho. Na tunatakiwa kuishi hivyo kwa sababu yote tunayoyafanya yana lengo la kuunganishwa kwa Mungu wa mianzo na miisho, ambaye na kwake tuliumbwa.
Ni vigumu kuishi na umilele kimtazamo. Maisha husinyaa mara kwa mara. Kuna nyakati ambapo inaonekana kwamba jambo la muhimu sana katika maisha ni kupita huu msururu wa magari, kushinda mabishano, au kutimiza tamaa ya ngono. Kuna nyakati ambapo furaha yetu na utoshelevu wetu husinyaa kupata vile viatu vipya au nyama inayopatika dakika kumi mbele. Kuna nyakati ambapo sisi tulivyo, Mungu ni nani, na wapi mambo haya yataenda kuishia nyuma ya mawazo, hisia, na mahitaji wa wakati huo. Kuna nyakati huwa tunapotea katikati ya habari ya Mungu. Tunapoteza akili zetu, tunapoteza uelekeo wetu, na tunapoteza kumbukumbu ya Mungu.
Mungu anatukumbusha kwamba hapo siyo mwisho, kwamba tuliumbwa na kuumbwa tena katika Kristo Yesu kwa ajili ya milele. Anatukumbusha tusiishi kwa hazina za kitambo: “Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;” (Mt. 6:19-20).
Fikiria juu ya hili: kama Mungu tayari amekutayarishia makao milele, kwa hiyo amekupa neema yote unayoitaka njiani, au hutafika huko. Kuna neema kwa ajili ya udhaifu wetu na mioyo inayoyumbishwa. Kuna msaada kwa ajili yetu na kukosa malengo. Mungu wa milele anakuoa neema yake ya milele ili uweze kuishi na mawazo ya milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.
More