Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwaka Mpya, Rehema MpyaMfano

New Year, New Mercies

SIKU 2 YA 15

Pumziko lako halipatikani katika kutambua hatima ya maisha yako, ila kwa kumwamini Yeye Pekee ambaye ameshatambua yote kwa ajili ya wema wako na utukufu Wake.

Tulikuwa njiani kuelekea kwenye soko la nyumbani pamoja na watoto wetu wawili wa kiume walipokua na miaka mitatu na wakauliza, "Baba, kama Mungu ameumba kila kitu, aliumba chuma za taa?" Nilipata wazo ambalo wazazi wote wanapata mara kwa mara wanapokutana na maswali yasiyoisha ya "kwanini" ambayo watoto wadogo huuliza. "Tunatoka hapa tulipo hadi pale tunapopaswa kuwa kwenye mazungumzo haya?" Au, "Kwanini ananiuliza swali la 'kwanini' kila saa?"

Binadamu tunashauku kubwa ya kujua na kuelewa. Tunatumia muda mwingi wa siku kwenye akili zetu tukijaribu kuelewa vitu. Hatuishi kwa silka. Hatuishi maisha yetu peke yetu. Sisi sote ni wanatheolojia. Sisi sote ni wanafalsafa. Sisi sote ni wanaikolojia tunaochimba mabwawa katika maisha yetu tukitaka kuelewa ustaarabu tuliombiwa ambayo ndio historia yetu. Huu mpango wa Mungu wa kutoa motisha unaambatana na zawadi nzuri za kiuchambuzi. Msukumo na zawadi hizo unatutenga na viumbe wengine wote. Ni utakatifu, ulioumbwa na Mungu ili tusogezwe karibu Naye, ili tupate kumjua na kujielewa wenyewe katika mfumo wa uumbaji wake na uamuzi.

Lakini dhambi zinafanya muamko na zawadi hii uwe wa hatari. Unatujaribu tufikiri kwamba tunaweza kuelewa mioyo yetu kwa kuelewa vyote. Ni swala la "kama ningeelewa hiki au kile, basi ningekuwa salama" aina ya maisha. Lakini haifanyi kazi. Katika wakati wako wa kipaji kizuri sana, bado utabaki na hali ya utata katika maisha yako; wakati mwingine hali ya utata wenye maumivu. Wote tunapita vitu vinavyotufanya tuelewe kidogo na havileta msaada mkubwa. Kwahiyo pumziko halipatikani katika kutaka kuelewa vyote. Hapana, pumziko hupatikana katika kumtafuta Yeye anayeelewa vyote na anayetawala vyote kwa utukufu wake na uzuri wetu.

Baadhi ya mistari yanaeleza vizuri pumziko zaidi kuliko Zaburi 62:5-7: "Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya. Tumaini langu hutoka kwake. Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana. Kwa Mungu wokovu wangu, Na utukufu wangu; Mwamba wa nguvu zangu, Na kimbilio langu ni kwa Mungu."

Katika wakati unapotamani kujua yale usiyoyajua, kunapumziko la kupatikana. Kuna Mmoja ajuaye. Anakupenda na anatawala vile usivyovijua akiwa na mawazo mazuri juu yako.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

New Year, New Mercies

Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.

More

Tungependa kushukuru Crossway kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:https://www.crossway.org/books/new-morning-mercies-hcj/